Maalim na turufu ya urais 2015

RAIS anayesaka ridhaa ya kuendelea kuongoza, Dk. Ali Mohamed Shein, anatumia jukwaa la kampeni kutetea mapinduzi ya Januari 12, 1964, kama vile kuna ubishani kwamba mapinduzi yale ni halali au haramu. Kwa hakika, jambo hili halijawahi kuwa la kubishaniwa hata kuwa ajenda wakati wa uchaguzi. Halikuwa mwaka 1995 ulipokuwa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi,…

Karibu tuijenge Zanzibar mpya

Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015 si uchaguzi wa kawaida kwa Zanzibar. Ni uchaguzi wa kihistoria. Utatupa Wazanzibari fursa ya kihistoria kufanya mabadiliko ya msingi ya jinsi tunavyoongozwa. Ni uchaguzi utakaoamua mwelekeo wa Zanzibar yetu.

Vikosi vya SMZ vitaundwa upya

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar ataviunda upya vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuvipatia vitendea kazi na kuimarisha maslahi yao.