Sanaa itumike kujenga amani

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, amesema sanaa ya muziki ina nafasi kubwa ya kuendeleza amani na maelewano duniani. Amesema kupitia sanaa hiyo wanamusiki kutoka pembe tofauti za dunia wamekuwa wakikutana kubadilishana uzoefu na kusoma tamadunia za kila upande, jambo ambalo husaidia pia kuzitangaza nchi na tamaduni zao…

Ichungeni amani iliyopo

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ametoa wito kwa Watanzania kuwa waangalifu na kuendeleza amani iliyopo, ili Tanzania isije ikatumbukia katika migogoro na machafuko kama inavyojitokeza kwa baadhi ya nchi za Afrika.

Maalim Seif ahudhuria sherehe za Muungano

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, alihudhuria sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika siku ya tarehe 26 Aprili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, sambamba na viongozi kadhaa wa kitaifa na kimataifa.

Jukumu la amani ni letu sote

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar inaunga mkono juhudi zinazochukuliwa na taasisi ya Kimataifa ya Global Peace Foundation katika kuhimiza amani na utulivu duniani.