Uendelezaji wa uwezo wa ndani

Zanzibar haina upungufu wa vipaji na watu wenye kujituma, bali ina upungufu wa uongozi wenye dira ya kuviendeleza vipaji na kuimarisha uwezo wa wananchi kujiletea maendeleo. Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF imejipanga kuuinua uwezo wa wananchi wa kawaida ili watumie vipawa na vipaji vyao kujenga maisha yao. Advertisements

Nina afya, nina uwezo – Maalim Seif

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ameuthibitishia ulimwengu kuwa yuko katika afya njema, baada ya kuongoza matembezi ya mazoezi kwa zaidi ya kilomita sita. Matembezi hayo yaliyoanzia eneo la Tungamaa hadi viwanja vya Mnazi mmoja Wilaya ya Wete, yamevishirikisha vikundi kadhaa vya mazoezi kutoka Mkoa wa Kaskazini Pemba. Akizungumza baada…

Donge, hongereni kwa kulima matikiti

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesifu juhudi zinazochukuliwa na wananchi wa Donge katika kuendeleza kilimo cha matunda na mboga mboga. Amesema iwapo kilimo hicho kitawekeza mikakati imara, kinaweza kuwa mkombozi wa kweli kwa wakulima na kuweza kuweza kuongeza kipato chao. Maalim Seif ameeleza hayo wakati akizindua uvunaji wa…

Maridhiano ndio roho ya Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ameshirikiana na viongozi wenzake wa juu wa nchi kuadhimisha Sikukuu ya Eid el-Fitr kufuatia kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ujumbe mkubwa unaowasilishwa kupitia ushirikiano huu wa viongozi wa juu hadharani ni kuwa Zanzibar inayahitaji maridhiano na umoja wake wa kitaifa. Kuyavunja…

“Tufuturuni pamoja kuimarisha mapenzi baina ya Waislamu”

Katika ratiba ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ya mwezi huu mtukufu, jana Jumatatu ya mwezi 6 Ramadhan 1436 ilikuwa zamu ya kufuturu pamoja na watendaji wa ofisi yake nyumbani kwake Mbweni. Futari hiyo ilizikutanisha pamoja jumuiya mbalimbali zikiwemo za Watu Wenye Ulemavu, Dawa za Kulevya, Ukimwi na Mazingira.…

Maalim Seif atembelea masoko

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema upungufu wa bidhaa katika masoko mbali mbali ya Zanzibar, umechangia kupanda kwa bei za bidhaa hizo. Amesema tofauti na Ramadhani iliyopita, Ramadhani hii kumejitokeza upungufu wa bidhaa zinazotumika zaidi kwa futari zikiwemo ndizi, viazi vikuu na majimbi, hali iliyochangia bei ya bidhaa…