“Ndiyo, nitaifanya Z’bar kuwa Singapore, na sitanii” – Maalim Seif

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, anakusudia kuuzindua rasmi mpango wake wa kuifanya Zanzibar kuwa Singapore ya Afrika Mashariki mwishoni mwa wiki hii. Alisema anapozungumzia mpango huo huwa hafanyi utani bali anazungumza akiwa na mikakati maalum ya kuweza kuibadilisha Zanzibar kufikia lengo hilo. Maalim Seif ambaye pia ni Makamu…

Ajira za kutosha chini ya CUF

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema wananchi wakimchaguliwa kushika wadhifa huo atahakikisha vijana kote Zanzibar wanapata ajira za kutosha na za heshima zitakazo wawezesha kuwa na maisha mazuri. Akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni katika jimbo la Kijini, Wilaya ya Kaskazini ‘A’ amesema uhaba wa ajira kwa…

Kima cha chini mshahara sh. 400,000

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema akichaguliwa atakuza uwezo wa Serikali kujiongezea mapato na ataongeza kima cha chini cha mshahara hadi kufikia 400,000. Akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni katika uwanja wa Masumbani jimbo la Chumbuni, Maalim Seif amesema Sera ya CUF imeonesha maeneo mengi ya kukuza…

CUF kujenga taifa lenye umoja, usawa na haki

Serikali itakayoundwa na kuongozwa na Chama cha Wananchi (CUF) baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 inakusudia kujenga taifa lenye umoja, usawa na haki bila ya ubaguzi wa aina yoyote, kwa mujibu wa mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi cha chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad. Akihutubia mkutano wa kampeni za chama hicho uliofanyika viwanja…

CUF itaipa nafasi ya juu sekta ya elimu

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema anakusudia kuiendeleza sekta ya elimu kwa kuongeza maslahi ya walimu na kuweka mazingira bora ya kusomea. Amesema hadhi ya elimu imeshuka Zanzibar, na kwamba iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao, atahakikisha kuwa sekta ya elimu inapewa nafasi yake…

Dk. Shein aeleze makambi ya masoksi yana kazi gani

CUF inamtaka Dk. Ali Mohamed Shein, iwapo kweli anataka wananchi wa Zanzibar wamuamini kwamba ana dhati ya kuhakikisha amani na utulivu, awaeleze wananchi kwa nini hadi leo hajachukua hatua zozote za kuyafunga makambi ya vijana wa CCM yanayoendesha mafunzo ya kiharamia ambayo Maalim Seif Sharif Hamad alimuandikia rasmi na hata kumueleza ana kwa ana juu…