Maalim Seif aisifu Azam TV

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesifu mchango unaotolewa na kampuni ya Azam, katika kukuza na kuendeleza sekta ya habari nchini. Amesema kampuni hiyo inayomilikiwa na mwekezaji mzalendo, imeonesha mafanikio makubwa tokea ilipoanzisha kituo cha televisheni cha (Azam TV) takriban miaka miwili iliyopita. Maalim Seif ametoa pongezi hizo wakati…

Ahsante Kitope

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewashukuru wanachama wa chama hicho katika Wilaya ya Kaskazini ‘B’ kwa kujitokeza kwa wingi na kuwa wastahamilivu kwenye mkutano wa hadhara wa CUF jimbo la Kitope, licha ya kuwepo kwa mvua kubwa. Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wanachama na…

“Hongereni Uturuki kwa kutunza historia yenu”- Maalim Seif

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameelezea kufurahishwa kwake na jinsi watu wa Uturuki walivyofanikiwa kutunza na kuenzi historia ya Taifa hilo. Maalim Seif alieleza hayo alipotembelea maeneo mbali mbali ya kihistoria katika mji wa Konya nchini Ututruki ambako alifika kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku tatu kuanzia…

Redio Noor kurudi upya

Jumuiya ya Al-Noor Charitable Agency, imesema kuwa inakusudia kuweka vifaa vya kisasa vya kudhibiti majanga ya moto kwa Radio Al-Noor FM, ili kujikinga na majanga hayo. Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya hiyo Sheikh Nadir Mahfoudh ameeleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad nyumbani kwake Mbweni, baada…

Polisi yaahidi ushirikiano na raia

Jeshi la Polisi nchini limesema litaendelea kushirikiana na raia katika jitihada zake za kukabiliana na vitendo vya uhalifu. Kauli hiyo imetolewa na  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, wakati akizungumza na Makamu wa Kanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ofisini kwake Migombani. IGP Mangu ambaye aliambatana na naibu…

Maalim Seif akutana na Mzee Mwinyi

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, leo amtembelea Rais Mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, nyumbani kwake Mikocheni, Dar es Salaam, ambapo viongozi hao wawili wamepata muda wa kuzungumza na kubadilishana mawazo juu ya masuala kadhaa. Maalim Seif alikwenda kwa Mzee Mwinyi, baada ya kufanya mazungumzo maalum na kituo cha Televisheni…