CCM inawatia khofu wananchi – Maalim Seif

Chama Cha Wananchi (CUF) kimekanusha taarifa zilizotolewa na badhi ya viongozi wa CCM kuwa Chama hicho kinakusudia kufanya vurugu kuanzia tarehe 22 mwezi ujao hadi siku ya uchaguzi.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi wa chama hicho katika viwanja vya Mkele Zanzibar.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.

Katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye pia ni mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema Chama hicho hakina sababu ya kufanya vurugu kwani tayari kina uhakika wa kushinda.

Maalim Seif ametoa ufafanuzi huo wakati akizungumza na wafuasi na wapenzi wa Chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika Pujini katika jimbo la Chonga kisiwani Pemba.

Amekishutumu Chama Cha Mapinduzi kuwa ndicho chenye mpango wa kuvuruga amani ya nchi kwani tayari kimeanza kutoa vitisho kwa wananchi kwa kuzungusha mizinga, kitendo ambacho kimeanza kuwatianza kuwatia hofu wananchi.

Amesema Zanzibar ni mali ya Wazanzibari wote, hivyo hakuna haja ya kuwatisha wananchi ambao ni raia halali wa Zanzibar.

Akichambua Ilani ya Chama hicho Maalim Seif amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar atatoa uhuru kwa wakulima wakiwemo wa zao la karafuu kuuza bidhaa zao mahali popote wanapotaka.

Amefahamisha kuwa serikali yake itatoa utaalamu, vifaa vya kisasa na mbegu bora kwa wakulima, ili kuwawezesha kuongeza uzalishaji na kujiongezea kipato.

Amesema pia anakusudia kutoa kipaumbele kwa kilimo cha viungo ambacho kinahitajika sana kwa soko la ndani na nje ya nchi.

Kuhusu Mapinduzi ya uvuvi, Maalim Seif amesema anakusudia kuwawezesha wakulima kuvua katika bahari kuu kwa kuwapatia vifaa vya kisasa na zana za kufanyia kazi zikiwemo boti za kisasa wa uvuvi.

Aidha amesema wakulima wa mwani watapatiwa bei nzuri ya kilimo hicho, sambamba na kuusarifu mwani ili kuungezea bei katika soko la ndani na nje ya nchi.

Mapema akizungumza katika mkutano huo, mratibu wa kampeni za CUF kisiwani Pemba Hamad Massoud Hamad amesema zoezi la uchukuaji wa kadi za kupigia kura lililoanza tarehe 28 mwezi limeingia dosari.

Amesema baadhi ya wapigakura katika vituo mbali mbali nchini wamerejeshwa na stakabadhi zao kwa madai kuwa vitambulisho vyao havionekani, na kupangiwa siku nyengine ambapo hawana uhakika wa kupata kadi hizo.

Amewataka wanachama waliokoseshwa kadi hizo kuorodhesha majina yao katika matawi yao, ili chama kiweze kufuatilia haki hiyo.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s