Zanzibar yenye mamlaka kamili ni neema kwa wote

Imani kubwa ya kihistoria tunayoendelea kupewa kupitia ridhaa ya wananchi inaturejesha tena kwao na mpango kazi uliotayarishwa kuirejeshea hadhi na heshima kwa nchi yetu pamoja na kuleta mabadiliko ya haraka ya kisiasa na kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya jamii nzima na taifa letu kuanzia tarehe 25 Oktoba 2015.

Zanzibar na mamlaka kamili

Zanzibar na mamlaka kamili

  1. Tutayarejesha Mamlaka Kamili ya Zanzibar kwa kuimarisha Muungano utakaozingatia Misingi ya Haki, Usawa na Heshima kwa nchi zote mbili zinazounda Muungano huu.
  2. Tutajenga Uongozi Mwema kwa Kuimarisha Misingi ya Uhuru, Haki na Maridhiano kwa wananchi wa Zanzibar
  3. Tutailinda, kuienzi, kuendeleza, kuijenga na kuiboresha misingi yote ya Umoja wetu wa Kitaifa ulioasisiwa na viongozi wetu wa kisiasa wa Zanzibar, Dkt. Amani Abeid Amani Karume na Maalim Seif Sharif Hamad tarehe 5 Novemba, 2009 na kupewa ridhaa na wananchi kupitia Kura ya Maoni ya tarehe 31 Julai 2010.
  4. Tutapambana kuondosha rushwa, ufisadi, upendeleo, uonevu, ubaguzi na woga ndani ya taasisi zetu pamoja na jamii kwa kurekebisha muundo wetu wa utawala, uwajibikaji, na utendaji katika kazi na utoaji wa huduma sambamba na kupanua viwango vya elimu na uelewa wa kutosha kwa jamii.
  5. Tutayaendeleza mashirikiano yetu ya kimataifa (International Relations and Cooperation) na majirani zetu, washirika wa maendeleo, taasisi, nchi wahisani na jumuiya mbali mbali za kimaendeleo kwa lengo la kuifanya Zanzibar inufaike na mahusiano na mashirikiano hayo. Mafanikio ya mashirikiano haya yatatokana na Zanzibar yenye mamlaka kamili ndani ya muungano wa haki, heshima na usawa.
  6. Tutatetea haki ya Zanzibar kushirikishwa katika Shirika la Kimataifa la Bahari (International Maritime Organization) pamoja na kusimamia kwa uwazi na kwa mujibu wa sheria za kimataifa mikataba na itifaki mbali mbali za Shirika la IMO ikiwemo suala la usajili wa meli (International Shipping Registry) na fursa zaidi kwa Wazanzibari katika uajiri melini.
  7. Tutasimamia na kuitetea haki ya Zanzibar katika sera, mipango na matumizi ya maeneo maalum ya kiuchumi ya bahari kuu (Exclusive Economic Zone) na yale ya madini ya chini ya bahari (Extended Constinental Shelf) kwa faida ya wananchi wa Zanzibar.
  8. Tutaingia kwenye uongozi tukiwa na dira ya mabadiliko itakayotupeleka kujenga mashirikiano ya kikanda katika sekta ya uvuvi wa bahari kuu (Regional Deep Sea Fisheries Management).
  9. Tutauondoa uonevu na ukiritimba unaofanywa na viongozi na watendaji wachache juu ya haki za msingi za wavuvi wetu wa mwambao na kuhakikisha haki na usawa kwa wavuvi wote ikiwemo wazalishaji wa mwani.

CUF Manifesto 2015

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s