Kima cha chini mshahara sh. 400,000

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema akichaguliwa atakuza uwezo wa Serikali kujiongezea mapato na ataongeza kima cha chini cha mshahara hadi kufikia 400,000. Akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni katika uwanja wa Masumbani jimbo la Chumbuni, Maalim Seif amesema Sera ya CUF imeonesha maeneo mengi ya kukuza…

Uendelezaji wa uwezo wa ndani

Zanzibar haina upungufu wa vipaji na watu wenye kujituma, bali ina upungufu wa uongozi wenye dira ya kuviendeleza vipaji na kuimarisha uwezo wa wananchi kujiletea maendeleo. Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF imejipanga kuuinua uwezo wa wananchi wa kawaida ili watumie vipawa na vipaji vyao kujenga maisha yao.

Dk. Shein aeleze makambi ya masoksi yana kazi gani

CUF inamtaka Dk. Ali Mohamed Shein, iwapo kweli anataka wananchi wa Zanzibar wamuamini kwamba ana dhati ya kuhakikisha amani na utulivu, awaeleze wananchi kwa nini hadi leo hajachukua hatua zozote za kuyafunga makambi ya vijana wa CCM yanayoendesha mafunzo ya kiharamia ambayo Maalim Seif Sharif Hamad alimuandikia rasmi na hata kumueleza ana kwa ana juu…

Manifesto ya CUF 2015

Mwaka 2010 tulifanya maamuzi sahihi ya kuanzisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kuchoshwa na migogoro ya kisiasa iliyodumu visiwani mwetu kwa zaidi ya miaka 50 sasa. Kinachohitajika sasa ni kuipatia Serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa uongozi unaojiamini na unaojituma ili kuwaletea Wazanzibari maendeleo waliyoyatarajia. CUF tumejiandaa kuwapa Wazanzibari uongozi huo. Kusoma manifesto…

Zanzibar yenye mamlaka kamili ni neema kwa wote

Imani kubwa ya kihistoria tunayoendelea kupewa kupitia ridhaa ya wananchi inaturejesha tena kwao na mpango kazi uliotayarishwa kuirejeshea hadhi na heshima kwa nchi yetu pamoja na kuleta mabadiliko ya haraka ya kisiasa na kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya jamii nzima na taifa letu kuanzia tarehe 25 Oktoba 2015.