Mradi wa MKUAJI, Kielelezo cha mafanikio Jimbo la Mtoni

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha mafunzo ya ujasiriamali Tanzania, kanda ya Zanzibar bibi Lucy Mwaipopo akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kuhusiana na bidhaa mbali mbali za wajasiriamali wa mradi wa MKUAJI. Wa pili kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni, Nassor Ahmed Mazrui

Mradi wa Kuendeleza Ujasiriamali na Ajira (MKUAJI), ni mradi wa wajasiriamali ulioanzishwa katika jimbo la Mtoni Wilaya ya Magharibi Unguja hivi karibuni. Wazo la kuanzishwa kwa mradi huo lilitokana na Mwakilishi wa Jimbo hilo la Mtoni Mhe. Nassor Ahmed Mazrui ambaye pia ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar. Continue Reading

Hamjambo wenyeviti na makatibu?

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad akielekea ukumbi wa mkutano katika hoteli ya Mazsons Mjini Zanzibar kwa ajili ya kufungua semina elekezi kwa wenyeviti na makatibu wa wilaya wa CUF

Maalim awaagiza viongozi kujenga chama

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mkurugenzi wa habari na haki za binadamu wa Chama hicho Salim Bimani baada ya kuwasili katika hoteli ya Mazsons Mjini Zanzibar kwa ajili ya kufungua semina elekezi kwa wenyeviti na makatibu wa wilaya wa CUF. Katikali ni mwakilishi wa Jimbo la mgogoni Pemba Aboubakar Khamis Bakari

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amewataka watendaji wa chama hicho ngazi  ya wilaya kufanya kazi kwa karibu na wanachama ikiwa ni hatua muhimu katika kukijenga chama chao. Continue Reading

Maalim Seif awatolea uvivu wanaogeuza siasa mradi wa biashara

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa (MKUAJI) katika shehia ya Mtoni Kidatu, Wilaya ya Magharibi Unguja. Kushotoni kwake (mwenye T-Shirt na kofia ya kapelo) ni Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.

Asema siasa ni fursa ya kuwatumikia watu

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad amesema siasa sio uwanja wa biashara bali ni fursa ya kuwatumikia wananchi, hasa katika majimbo ya uchaguzi. Alisema kwa kuzingatia kuwa kuingia katika siasa ni fursa ya kuwatumikia wananchi, viongozi wa kuchaguliwa lazima wajenge utaratibu wa kushikikiana kwa karibu katika kufanyakazi za kuwakomboa wananchi kutoka katika umasikini. Continue Reading